Ukiacha mbali muziki ambao ndio ulioanzisha safari yake mpaka hapa alipo, ni Mbunge aliyeshinda uchaguzi uliopita kwa kura nyingi kupita Mbunge mwingine yeyote. Aliweka rekodi. Rekodi hiyo haikuja kirahisi. Tunaweza kusema ilitokana na utendaji wake. Yasemekana ni miongoni mwa wabunge walio karibu na wananchi wake kuliko mwingine yeyote. Anajua kwanini wamemchagua. Hataki kuwaangusha.
Huenda ndio maana hivi karibuni aliamua kurudi studio kuwakumbusha wapiga kura wake na mashabiki wake kwamba hajasahau alipotoka. Akaingia studio MJ Records kurekodi Freedom. Hii hapa ni video ya Freedom