Miongoni mwa nyimbo/video ambazo zimesubiriwa kwa hamu mwaka huu ni pamoja na hii. Ushirikiano wa Diamond Platinumz na P-Square ni jambo zuri. Wote ni wanamuziki wenye jina barani Afrika na hata nje.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoambatana na wimbo huu, mikono na akili za wengi zimesheheni. Umeandikwa na Diamond Platinumz na P-Square wakiwa jijini Lagos tarehe 10 January 2015 ndani ya Square Records.
Beat ni kutoka kwa SHIRKO kutoka Tanzania kisha ikachanganywa na V-Teck kutoka Nigeria na kuongezewa vionjo na Laizer kutoka Wasafi Records-Tanzania. Video Imetengenezwa na Godfather jijini Johannesburg, Afrika Kusini.