Kuna kitu ambacho kinanivutia sana kuhusu muziki kutoka kwa Shaa hususani tangu alipoamua kufanya muziki ambao mimi nauita “wa kwetu”. Ni aina fulani ya muziki ambayo naamini kama tungeamua kuipa nafasi isingetulaza kama tumekunywa klorofomu.
Ila hayo tutatafuta muda tuyaongelee. Ngoja kwanza nawe usikilize “Sawa” kutoka kwa Shaa. Sawa eenh!